Thursday 20 March 2014

Tuhuma kutoka kwa Mabeste juu Ya B Hits


MABESTE AWATOLEA UVIVU B HITS.

MMOJA KATI YA WASANII BORA KATIKA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA {BONGO FLEVA}MABESTE VENANCE,AMEAMUWA KUWATOLEA UVIVU,WAMILIKI WA RECORD LABO YA B HITS,HII NI BAADA YA UONGOZI WA LEBO HIYO KUANZISHA TUHUMA JUU YA MSANII M RAP{LION}
ALIYEWAHI KUWA CHINI YA LEBO YAO,HII NI KUTOKANA SINGO MPYA ALIYOIACHIA MSANII HUYO "M RAP-"Usiende Mbali Feat JUX",SINGO ILIYOPIKWA CHINI YA STUDIO ZA AM RECORDS YAKE MANECKY ,TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA B HITS NI JUU YA SINGO HIYO KUDAI KUWA WAO NDIYO WAMILIKI SAHIHI WA SINGO HIYO,B HITS WAKISISITIZA HILO KUPITIA PRODUCER WA STUDIO HIZO"PANCHO LATINO"
ALIYEDAI KUWA YEYE NDIYE ALIYEIPIKA SINGO HIYO WAKATI M RAP AKIWA CHINI YA STUDIO HIZO,AKISISITIZA KUWA M RAP AMETUMIA UJANJA WA KUIBADILISHA SINGO HIYO JINA TOKA "Only You" NA KUIPA JINA LA "Usiende Mbali"
TUHUMA ZILIZOPINGWA NA MABESTE AKIDAI SABABU ALIZODAI PANCHO SI ZA MSINGI KITAALUMA,MABESTE AMEFUNGUKA KUPITIA ACC YAKE YA FACEBOOK MCHANA WA LEO AKIANDIKA KAMA IFUATAVYO,"Nasikitika Pancho Latino na Uongozi wa Bhits kwa kulalamika kua M-Rap ametumia mistari yao katika Track yake aliyoifanya Am Records (usiende mbali) kuwa ametumia Verse alizowahi kuandika kipindi yuko Bhits na kuamua kutoa hiyo Track yenye hiyo Verse ambayo ni (only you remix)... sasa mbona (only you remix) waliyoitoa Bhits ile chorus aliyoifanya Jux niliandika mimi wakat niko Bhits!! Je mbona wao wametumia mistari yangu wakati mimi siko Bhits? Na kama issue ni Copy n Paste au kuishiwa na idea,mbona beat iliyotumika kwenye Track yangu ya "SIRUDI TENA" Pancho amei Copy kwenye Track ya (cheap monkey ft chriss brown - champion)?? Je ni haki wanachofanya??
Ama wanataka kumuaibisha tuu dogo(M-rap), mbona wao pia wanazingua nao???

#MabesteArmy!.....ANAMALIZIA MABESTE,

AWALI MWANZONI MWA MWEZI HUU MSANII MDOGO ANAYEFANYA POA KWENYE GAME LA MUZIKI BONGO M RAP{LION}ALIAMUA KUJITOA KWENYE LEBO YA B HITS ILIYOKUWA IKISIMAMIA KAZI ZAKE,HUU UKIWA NI MUENDELEZO WA KUJITOA KIMKATABA KWA BAHADHI YA WASANII WALIOKUWA WAKISIMAMIWA KAZI ZAO NA LEBO HIYO,
WASANII WALIOTANGULIA KUJITOA KWENYE LEBO HIYO NI PAMOJA NA VANESSA MDEE"VEE MONEY" PAMOJA NA MABESTE,
KATIKA KUKUPA MLINGANYO WA MAAMUZI KWA UPANDE WAKO ZISIKILIZE NGOMA  ZOTE MBILI,ILIYOTENGENEZWA B HITS NA HII YA AM RECORDS


by omaryramsey

No comments:

Post a Comment