Kupitia ‘Planet Bongo’ ya East Afrika Radio amesema hana taarifa yoyote
aliyopokea kutoka BASATA kuhusu kufungia wimbo wake, Amesema
“Sina jibu la moja kwa moja na napata kigugumizi kwa sababu sina
taarifa rasmi kwa kweli, yani finaly mimi nakuwa kama shabiki tu tena,
vile shabiki alivyoona ndivyo mimi kama Roma nilivyoona, niliamka tu na
mimi nikaona kama kuna chombo kimoja cha habari kimepost katika akaunti
ya Instagram, kwamba kuna tamko limetoka BASATA kwamba limefungia nyimbo
ya Roma, kwa sababu ambazo walizianisha” - Roma
Aliongeza kuwa pia hafamu utaratibu unaotumiwa na BASATA katika kufikisha taarifa kama hizo kwa wasanii
“Nisiwe muongo sijui taratibu kinakuwa kinatumia kufikisha
information zao, kwa sababu kitu ambacho naona ingekuwa rahisi kama
artist kabla hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya
sanaa, iwe inawasilishwa katika hiko chombo, nadhani hapo tungekuwa
tunaenda sawa” - Roma
Kwa upande wa pili, Afisa Habari wa BASATA Bwana Aristide Kwizela amesema kuna aina mbili ya kufikisha taarifa hizo
“Kuna kufungia kwa maana ya msanii mwenyewe kuandikiwa, lakini kama
kuna taarifa imetoka public kwamba nyimbo za namna hiyo zimezuiliwa,
kuna two way either barua kuandikwa kwa msanii au pia kuna public
anouncements kwamba wimbo fulani umefungiwa” - Kwizela.
Source: EATV
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment