.
SHINDANO la kusaka vipaji vya muziki,
Bongo Star Search (BSS) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 9, limeongeza
zawadi ya mshindi wa shindano hilo ambapo sasa atajinyakulia shilingi
milioni 60, ambapo shilingi milioni kumi zitapelekwa studio kwa ajili
ya kusaidia shughuli za kurekodi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa
habari, Jaji Mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’, alisema
kuwa shindano hilo lina msisimuko wa kipekee kwa kuwa washiriki wote
ni wazuri kiasi majaji wanapata wakati mgumu kumchagua mshindi.
“Mshindi wa shindano hili ataondoka na
sh. milioni 60, katika kinyang’anyiro cha safari hii chenye msisimko
mkubwa hadi hata sisi wenyewe tunapata wakati mgumu kama majaji,”
alisema Ritha
Fainali za shindano hilo zinatarajiwa
kufanyika Ijumaa Oktoba 9 Mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon
uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam. Siku hiyo pia
kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria
ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Gallardo.
“Ukiachia mbali msanii huyo pia kutakuwa
na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Bendi, Nevy Kenzo ambao
watakamua sambamba na wasanii mahiri ambao ni zao la BSS kama Peter
Msechu na Kala Jeremiah.
Viingilio siku hiyo vitakuwa 25,000/=, VIP 50,000/= na VVIP 100,000/=
Nawaomba mashabiki waje kwa wingi maana fainali ya mwaka huu ni ya
kipekee kabisa,” alisema Madam Ritha.
-Globalpublishers
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment