Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha ‘East Africa radio’ Nikki
amesema kutokuwepo kwa umoja wa wasanii mambo mengi yatazorota, hivyo ni
lazima kuwe na umoja utakaosimama na kuwatetea wasanii
“Umoja ni kitu cha msingi, kwa sababu bila umoja mambo mengi ya
wasanii yatazorota, na kutokuwepo kwa umoja kutatengeneza matundu ambayo
wajanja wachache watapitisha mikono yao kwenye hayo matundu na
watafaidika nayo, kwa hiyo lazima kuwe na umoja wa wasanii, ambapo
utasimama na kuwasemea wasanii”
Pia alitolea mfano wa matokeo waliyopata baada ya wasanii kuungana kipindi cha Katiba, Alisema
“Wasanii wengi pia hawaoni umuhimu wa umoja, kwa hiyo wamekosa
msukumo wa kuwa na umoja, na pia chama na chenyewe kimekuwa kimezidiwa
sana na kutokuwepo kwa umoja wa wasanii, kwa hiyo kimejikuta nguvu zake
zimekuwa chache, lakini umoja ni kitu cha msingi sana, kuna mifano mingi
kama wasanii tulivyo ungana tukatoa sauti zetu kwenye katiba tukaona
matokeo yake, kwa hiyo mambo mengi ya wasanii yataweza kurekebishwa
kukiwa kuna umoja”
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment