Rapper wa nchini Marekani, 50 Cent inasemekana huenda akakutana na mkono wa Sheria kutokana na tukio alilolifanya wiki iliyopita katika tamasha Baltimore la kumpiga shabiki wake wa kike maeneo ya kifuani.
Kwa mujibu wa TMZ, mwanadada alishambuliwa na 50 cent aliyejulikana kwa jina la Donnetta Derr, Baada ya kutoka hospitalini kucheki Afya ya mwili wake alienda kwa mwanasheria wake.
Wakati huo huo, 50 hivi karibuni katika ukurasa wake wa Instagram aliandika ” I’m gonna let POWER return on my birthday. This season is even better then the last. Make sure you put STARZ in your cable package. POWER, BMF, Tomorrow Today. Coming soon!!! “
Asilimia kubwa ya wapenzi wa mziki nchini marekani masikio yao yote yanangoja kusikia kauli ya mwanadada Derr, kama atamfungulia kesi 50 au atapotezea ?
No comments:
Post a Comment