Msanii wa muziki wa hip hop Kala Jeremiah, amefunguka na kudai alishtushwa na kauli tata kutoka kwa msanii mwenzake Dayna
Nyange.
Kauli hiyo ya Dayna Nyange ambayo aliitoa mbele ya Tv ambapo alidai kutomfahamu Kala Jeremiah lakini alikuja kupuuzia
baada ya kugundua alisema ki masihara japo hajawai kumuuliza.
Kala Jeremiah amesema awali watu
walipomwambia alishtuka na hakuamini lakini baada ya kutazama marudio ya
kipindi aligundua Dayna aliongea kwa utani na wala hakutegemea kama
ingekuwa ni story kubwa na kusisistiza kuwa wao ni washkaji hakuna hata
ugomvi unaoendelea kati yao.
"Sitaki kuamini kama Dayna
hanifahamu. Sisi ni washkaji wa muda na hata alivyodai hanifahamu huwezi
amini sijawahi kumpigia simu nimuulize maana tunakutana na tunapiga
story kama kawa. Hicho siyo kitu kikubwa sana kwangu cha ku-mind kwa
nini anikane, kwa sababu kwanza kila mtu anajua ushkaji wetu uliopo kati
yangu mimi na Dayna na ukizingatia mimi ni mmoja kati ya marafiki zake
wanaoimba hip hop" Amesema Kala Jeremiah kwenye eNewz.
No comments:
Post a Comment