Wakiwa nyumbani kwao Dortmund walikubali kipigo cha mabao 3 kwa 2 
toka kwa wakali wa Ufaransa Monaco. Mchezo ambao ulipaswa kuchezwa siku 
ya Jumanne lakini kutokana na mlipuko wa bomu karibu na basi la Dortmund
 ukapigwa Jumatano.
Kocha wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel amesema kipigo toka kwa 
Monaco lawama ziwaendee UEFA. Tuchel anadai baada ya tukio la mlipuko, 
chama hicho cha soka cha Ulaya kililichukulia tukio hilo kikawaida sana 
na wala hawakuipa Dortmund umuhimu mkubwa.
Tuchel anasema kikosi chake hakikuwa tayari na mchezo kupigwa siku ya
 Jumatano kwani wachezaji hawakuwa sawa kiakili, lakini UEFA badala ya 
kukaa chini wao kama wahanga wa tukio na kuwauliza nini cha kufanya?FIFA
 walifanya maamuzi wenyewe bila kuwashirikisha.
“Hawakutuuliza nini cha kufanya, walikaa wenyewe wakafanya maamuzi 
kisha baadae wakatutumia ujumbe kwamba mechi itachezwa siku ya Jumtano, 
ilitunyong’onyeza lakini hatukuwa na jinsi lakini kitendo cha mechi 
kupangwa bila kutushirikisha haikuwa sawa” alisema Tuchel.
Kauli ya Tuchel inapingana na kauli ya awali ya UEFA ambao walisema 
kabla ya mchezo huo kwamba, baada ya tukio la mlipuko kutokea waliwaita 
Monaco na Dortmund na kukaa nao chini ambapo walikubaliana kwa pamoja 
kwamba mchezo urudiwe siku inayofuata.
Kipigo cha nyumbani kutoka kwa Monaco kimeiweka katika hatari ya 
kutolewa katika Champions League, lakini Tuchel anaamini hiyo ilikuwa 
kama kipindi cha kwanza na cha pili ni nchini Ufaransa watapambana ili 
kusonga mbele.

 
No comments:
Post a Comment