Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya
AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden, Thomas Ulimwengu
atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu akiuguza jeraha
la goti.
Ulimwengu aliyejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa mwezi Januari
alipata majeraha hayo mwezi uliopita hali iliyopelekea akose mechi mbili
za kirafiki za Stars dhidi ya Botswana na Burundi licha ya hapo awali
kuitwa na kocha Jackson Mayanja.
Katika Interview wiki hii na Times FM kupitia kipindi cha Wizara Ya Michezo imezungumza na
mshambuliaji huyo kutoka nchini Sweden, ambapo alisema ameelezwa na
daktari kuwa atalazimika kukaa nje kwa majuma 12 ili aweze kurejea
katika hali yake.
“Niliumia wiki kadhaa zilizopita na ni kama vile nilipona nikaanza
mazoezi ndipo nikajitonesha, sasa nimetoka kwa daktari hapa muda huu
ameniambia nipumzike kwa miezi mitatu ndipo nitakuwa fit,” alisema
Ulimwengu.
Tayari Ulimwengu ambaye alishaanza kuonyesha makeke mazoezini na
katika mechi za kirafiki amekosa mechi mbili za ligi kuu nchini humo
ambayo imeanza hivi karibuni na majeraha haya yatamfanya akose mechi
nyingi zaidi.
No comments:
Post a Comment