Mzazi mwenziye na Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’, Siwema Hudson amesema kitendo cha serikali kumpa kashikashi
kutokana na wimbo wake wa Wapo hakikumshangaza kwani alitarajia hayo
yatokee kwa kuwa zilipendwa wake huyo ni mtu wa kukurupuka.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa juzi baada ya Nay kutoka polisi, Siwema
alisema yeye amekaa na Nay kwa muda mrefu na mara nyingi akiamua jambo
ndiyo hivyo wala hakuna mtu anayeweza kumshauri.
“Unajua Nay anapenda kukurupuka na wala hataki mtu apinge wazo lake,
kama ameamua kufanya kitu anafanya tu na nilifahamu kuwa ipo siku hilo
lingemtokea, sasa kama limepita anatakiwa kujitathmini upya,” alisema
Siwema
No comments:
Post a Comment