Friday 31 March 2017

Alex Iwobi atoa mawazo haya juu ya Wenger ndani ya Arsenal


Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria na klabu ya Arsenal Alex Iwobi, amesisitiza suala la kutaka kuona meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger akisaini mkataba mpya.

Iwobi ni mmoja wa wachezaji wanaopingana na baadhi ya mashabiki wanaoongoza mkakati wa kuushinikiza uongozi wa Arsenal usimpatie mkataba mpya meneja huyo kutoka nchini Ufaransa.

Iwobi amesema mpango huo sio sawa, na hadhani kama utakua na mantiki yoyote mbele ya viongozi wa The Gunners. ”Ni mtu sahihi kwa mawazo yangu,” alisema Iwobi mwenye miaka 20.”Ningelipenda abakie.”

Wenger mwenye umri wa miaka 67 amekuwa akipingwa na baadhi ya mashabiki wa Arsenal, baada ya kikosi chake kushuka mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya England kufuatia kufungwa katika michezo mitano iliyopita.

Magoli 10-2 ikiwa ni uwiano waliofungwa na FC Bayern Munich katika michuano ya Ulaya imeongeza msukumo kwa meneja huyo kupingwa.

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini amepewa ofa ya kuongeza miaka miwili.

No comments:

Post a Comment