Baada ya Kemistri yao kwenda vizuri na kushika nafasi ya juu katika chati tofauti Duniani kupitia wimbo wa One Dance, Wizkid amemvuta tena upya Drake kwenye ngoma ya “Come Closer,” ambayo mara ya kwanza iliitwa jina la “Hush Up the Silence.”
Come Closer ilivuja mtandaoni January ikiwa kama “Hush Up the Silence.” Wizkid ameamua kuachia version ya mwisho ya wimbo huo ambao utakuwa katika Album mpya ya Wizkid ya Sounds From the Other Side.
Tukiwa bado tunaisubiria video ya wimbo huo ambao inatarajiwa kutoka muda wowote kuanzia sasa, nikufahimeshe kwamba ambaye katengeneza video hii ya “Come Closer” ndie Director aliyetengeneza video ya Migos “Bad and Boujee”, “No kissing” ya Patoranking, “King Kunta” Kendrick Lamar kama msaidizi, anafahamika kama Daps.
Daps ni Mnaijeria ambaye amekulia UK na anafahamika kwa jina kamili kama Dapo Fagbenle, ameshatengeneza video kibao za Afrika pamoja na America, kikubwa kingine huwa pia anaandaa Concept za video kibao ikiwemo “Fancy” ya Iggy Azelea, ambazo zote zilitumika na Director X.
No comments:
Post a Comment