Friday, 31 March 2017

FIFA yakubali kuwepo timu 48 kombe la dunia

 


Baada ya Rais mpya wa FIFA, Gianni Infantino kutaka kuwepo kwa timu 48 ambayo ilikua ni moja ya ahadi zake katika kampeni.

Chama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020. FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.

Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema. Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.

Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.

Mapendekezo hayo yapo hivi

Afrika – 9 kutoka timu za awali 5

Asia – 8 kutoka timu 4 za awali

Ulaya – 16 kutoka timu 13 za awali

Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean – 6 kutoka timu 4 za awali

Bara la Oceania – 1 kutoka timu 1 ya awali

Amerika ya Kaskazini – 6 kutoka timu 4 za awali


Mwezi januari chama hicho chenye mamlaka makubwa ya soka duniani, kilipanga kuongeza timu zitakazo shiriki michuano ya kombe la dunia kutoka 32 mpaka 48 na hii itaanza mwaka 2026.

Source: BBC

No comments:

Post a Comment