Wednesday, 29 March 2017

Sanchez: Nilikuwa kipa timu ya jela



Nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez amesema kwamba wakati anakua alikuwa anacheza nafasi ya golikipa kwenye timu ya jela.

Sanchez ambaye maisha yake ya soka kwenye dimba la Emirates yamekuwa njiapanda, amekuwa miongoni mwa washambuliaji bora duniani akianzia Udinese, Barcelona, Chile pia ndani ya kikosi cha Washika Bunduki wa London.

Anasema kwamba matarajio yake kwenye maisha ya soka yamekuwa tofauti na awali alipokuwa kijana mdogo kwani alidhani angeendelea kuwa golikipa.

“Nilikuwa ninahitaji niwe mchezaji wa kulipwa tangu nikiwa mdogo,” alisema mshambuliaji huyo wa Arsenal mwenye miaka 28.

“Nilicheza mpira mtaani, lakini mara nyingi nilipenda kwenda katika jela iliyo karibu na nyumbani. Tulicheza na watu ambao waliokuwa wameshindikana  na nilicheza golini kama kipa.”

No comments:

Post a Comment