Rapa ambaye wimbo wake wa ‘Wapo’ unazungumzwa zaidi kwa sasa kwenye
mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari, Emmanuel Elibariki
(Nay wa Mitego), amesema kwa sasa anajipanga ajue cha kuzungumza na Rais
Magufuli kama atapata nafasi ya kukutana naye kama alivyomuagiza.
Ney alisema alipotoa wimbo wake huo alijua hautafurahiwa na watu wote,
lakini kwa sasa anashukuru kuwa huru, na sasa anafikiria cha kuzungumza
na Rais kama atapata bahati ya kukutana naye.
Akizungumza na Gazeti la Mtanzania wiki hii, Nay alisema "Kwa sasa nafikiria mwaliko wa Rais wa kukutana naye, lakini pia kama
nitakutana naye nitamweleza kuhusiana na malengo ya wimbo wangu na namna
wananchi wanavyomzungumzia huku mitaani,".
Baadhi ya nyimbo za msanii huyo zilizowahi kufungiwa kutokana na madai
mbalimbali, ikiwamo ya kukiuka maadili ni ‘Shika Adabu Yako’ aliowaimba
baadhi ya wasanii wenzake, ‘Pale Kati’ uliodaiwa kuwadhalilisha
wanawake. Pia wimbo wa ‘Itafahamika’ alioimba baadhi ya wasanii wenzake
uliwahi kumletea matatizo na baadhi ya wasanii wenzake waliomwelewa
tofauti na malengo yake alipotoa wimbo huo.

No comments:
Post a Comment