Kiungo wa Liverpool Adam Lallana ataukosa mchezo wa ligi kuu ya
England mwishoni mwa juma hili dhidi ya Everton (Merseyside derby),
kufuatia jeraha ya paja linalomkabili kwa sasa.
Lallana alipatwa na maumivu ya paja wakati wa mchezo wa kuwania
kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Lithuania uliochezwa mwishoni
mwa juma lililopita kwenye uwanja wa Wembley, ambapo England walichomoza
na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa, Lallana anakadiriwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha mujuma manne.
Hata hivyo jopo la madaktari wa Liverpool lipo katika shughuli ya
kumpatia tiba kiungo huyo ili kuangalia uwezekano wa kupunguza muda wa
kukaa nje ya uwanja.
Mcheza mwingine wa Liverpool ambaye ana hatihati ya kucheza mchezo
dhidi ya Everton mwishoni mwa juma hili, ni nahodha na kiungo Jordan
Henderson anaesumbuliwa na maumivu ya mguu, huku kukiwa na taarifa njema
za kurejea kwa Philippe
Coutinho na Roberto Firmino baada ya kumaliza mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za kombe la dunia dhidi ya Paraguay uliochezwa leo alfajiri.

No comments:
Post a Comment