Daily Star, linasema mechi kati ya Arsenal ma Man
City mwishoni mwa wiki inaweza kuamua hatima ya kocha Arsene Wenger,
Inter Milan wanaweza kumtoa Gabriel Barbosa ambaye anatakwa na Liverpool
kwa mkopo. Inter Milan wanaangalia jinsi ya kumrudish mlinzi wa
Manchester United Matteo Darmian katika ligi ya Serie A, Manchester
United na Arsenal wanapigana vikumbo kumsajili nyota wa Villareal Samuel
Castillejo, imeripotiwa kwamba Chelsea wanataka kuwapa PSG Diego Costa
ili wapewe Javier Pastore.
The Sun, Antonio Conte amemuweka Alexis Sanchez
katika orodha ya nyota anaowataka sana kipindi cha usajili. Chelsea
wanajipanga kumpa Eden Hazard £300,000 kwa wiki ili kujaribu kumzuia
asiende Real Madrid. Manchester United wanajipanga kutuma dau la £40m
kujaribu kumsajili Eric Dier wa Tottenham Hotspur. Beki wa zamani wa
Mamchester United Paddy McNair amedai kwamba alilazimisha uhamisho wake
kwenda Sunderland.
Daily Mirror, Erik Lamela na Mousa Sissoko ni
wachezaji ghali katika timu ya Tottenham lakini wote wawili wanahusishwa
na kutimkia Italia msimu ujao. Raisi wa Houstom Dynamo amemuonya Wayne
Rooney kwamba asitegemee mteremko kama akihamia katika ligi kuu ya
nchini Marekani. West Ham wanamuona Rafael Benitez kama mrithi wa Slaven
Billic endpo watashindwana naye.
Daily Express, gazeti hili leo limekuja na habari za
Manchester United moja inasema Zlatan Ibrahimovich amedokeza kuhusu
kubakia United msimu ujao na pia Manchester United wanataka kumsajili
kinda wa Ufaransa ambaye pia anatafutwa na Real Madrid Aliou Traoure.
Daily Mail, Manchester United wanamfuatilia kwa
karibu kinda wa Celtic Kiernay Tierney ambaye ameanza kuwa gumzo kubwa.
Harry Kane anaweza kurejea mapema zaidi ya ilivyotarajiwa katika kikosi
cha Tottenham. Ronaldinho Gaucho ameachia wimbo wake wa kwanza na wimbo
huo unaitwa Sozinho.
Dailly Telegraph, gazeti hili linasema klabu ya West
Ham hadi sasa haina mpango wa kumuongezea mkataba kocha wao Slaven
Bilic kutokana na matokeo ya hivi karibuni. Mmiliki wa klabu ya
Sunderland amemuambia David Moyes kwamba asiwe na wasiwasi kwani hata
timu hiyo ikishuka daraja bado ataendelea kuwa kochwa wao.
The Independent, gazeti hili lina habari isemayo
Alexis Sanchez alipokuwa mtoto alikuwa akitembelea jela nchini kwao ili
akacheze mpira. Kocha Diego Simeone amesema Antoine Griezman hazuiliwi
kuondoka Atletico Madrid.

No comments:
Post a Comment