Tuesday 28 March 2017

Ruby atokwa na povu kwa kichwa hiki cha habari cha gazeti la Udaku


Siku chache tu zimepita baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza kuwa waandishi wa habari hawatakuwa na uhuru wa kujiachia basi haya huenda yakaungwa mkono hata Ruby kwani kachoshwa na magazeti ya Udaku.

Ruby kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha ya ukurasa wa gazeti wenye headline iliyosomeka “Ruby Daladala kwake ni mwiko” baada ya kuona kichwa hicho cha habari ndiyo akaona ni vyema awape makavu wamiliki wa gazeti hilo la udaku kwa kuandika.


“Kwani jaman mkikosa vya kuandika mkatulia mnakufaa?acheni kuandika ujinga kama huu …hili gazeti linajijua plz tuheshimiane sana mm ni binadamu tu wakawaida hata toroli ntapanda mkoooomeeee kuniandika uongo mmxiiiuuueeee kama sapoti nainipite tu lakin shobo za kijinga staki …lini mmefanya interview na mm nikasema hayo maneno?!mngemalizia kabisa basi Ruby kaburi kwake ni mwiko alafu mje mnizikie baharini?!….huu ni ushamba mmxiiiuueee next time take care make sure#magazeti ya kiki za kijinga sitaki”Ameandika Ruby.

No comments:

Post a Comment