Mwanadaada mwenye umbo matata anayesumbua kunako Tasnia ya Muziki Bongo na Filamu,
Snura Mushi ‘Snura’ amesema kuwa yeye ni mwanamke mwenye wivu sana
jambo ambalo limemsababisha mpaka kushindwa kut oka kimapenzi na
mastaa wanaomtaka.
Akipiga stori mbili tatu na Uwazi Showbiz,
Snura aliongeza kuwa amekuwa akifuatilia uhusiano wa kimapenzi wa
mastaa wengi na kugundua kuwa huwa haudumu kutokana na mastaa kutokuwa
waaminifu au mazingira ya kazi zao ambayo kwa wasanii wa kiume
yanawafanya kuwa karibu na wanawake jambo ambalo kwake hawezi
kulivumilia maana atahisi tu anasalitiwa.
“Naomba
niwe muwazi, kwa sasa sitamani kabisa kutoka kimapenzi na mtu maarufu au
niseme tu staa kutokana na mimi kuwa mtu mwenye wivu sana, unajua
mastaa wengi wa kiume huwa karibu sana na wanawake kwa mazingira ya
kawaida ya kikazi, sasa mimi nikiona hivyo ninafahamu ninasalitiwa tu,” alimaliza Snura.
No comments:
Post a Comment