Tuesday 28 March 2017

Drake adaiwa kupiga chini show yake ya Amsterdam baada ya kuugua


Drake alikuwa amepanga kutumbuiza show mbili Jumanne hii huko jijini Amsterdam, Uholanzi, lakini amelazimika kusitisha katika dakika za mwisho baada ya kudaiwa kuugua. Madaktari wake walidaiwa kumuomba asitumbuize.

Muda mfupi baada ya kusitisha show hiyo, tetesi zilianza kusambaa kwamba rapper huyo aliugua baada ya kuvuta bangi nyingi backstage. “They said Drake smoked too much weed backstage and threw up so much he went to the hospital and cancelled his show via @arminshh,” ameandika DJ Akademiks.

Hata hivyo vyanzo vilivyo karibu na rapper huyo vimethibitisha kuwa aliugua kweli na wala si sababu ya kuvuta bangi.

No comments:

Post a Comment