Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann,
ameitakatisha tamaa Manchester United inayotajwa kuwa katika harakati za
kumsajili mwishoni mwa msimu huu, kwa kusema hana mpango wa kuondoka
mjini Madrid kwa sasa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amekua chaguo la kwanza la
Jose Mourinho kuelekea usajili wa majira ya kiangazi, lakini kauli yake
ya kusema bado ni mwenye furaha huko Vicente Calderon inafuta harakati
hizo.
“Mustakabali wangu? Binafsi ninategemea kuuonyesha uwanjani na sio
sehemu nyingine katika maisha yangu, sina mpango wa kuondoka Atletico
Madrid na ninafurahia maisha ya klabu hii,” Griezmann aliiambia
Telefoot. “Ninasisitiza tena, ninafurahia maisha ya mji wa Madrid. Hakuna kitakacho badilisha msimamo wangu.
Juma lililopita meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone aliwaambia
waandishi wa habari kuwa, hatompangia wala kuweka msimamo kwa
mshambuliaji huyo kubaki au kuondoka klabuni hapo.
Alisema Atletico Madrid ilishawahi kuwa na washambuliaji waliosiofika
duniani kama Sergio Aguero, Falcao na Diego Costa lakini waliondoa
Vicente Calderon.
No comments:
Post a Comment