Friday, 16 October 2015

Uongozi wa MDB wampiga chini Young dee, wadai kuwa akiendelea na tabia yake ataishia pabaya

Uongozi wa Kampuni ya Million Dolla Boyz unaomiliki studio za ‘Aunthentic records’ na uliokua unasimamia kazi za Young dee umempiga chini msanii huyo kwa madai ya kutokua na shukrani na tabia mbaya.

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM, CEO wa Kampuni hiyo, Millian amesema amesikitishwa kusikia kuwa Young dee anasema wamemkataza kufanya kazi na Mtu chee

“Naskia oh anasema oh  management yangu imeniambia nisifanye kazi na mtu chee, we dont.. hatu’run maisha ya dee kabisa, we dont manage him.. i can not be with him, i can not manage him, na maisha yake na takataka yake nimemwambia mimi fanya mambo yako utajua mwenyewe, i have tried my best me nimemlea dee i have done soo much”  

Millian amedai pia sababu nyingine ya kumpiga chini ni kuhusiana na kujihusisha na madawa ya kulevya . Hata hivyo Young dee amekataa kuzungumzia suala hilo.

 

Millian pia aliandika ujumbe mrefu kwenye mtandao wa Instagram kuhusiana na kuacha kujihusisha
“Ulipokuwa huna nilikuona, nikakuhurumia na kukusaidia. Sikuwahi kukudai pesa hata shilingi moja kwa yote nilokusaidia. Nilikutungia nyimbo Ambazo zilikurejesha kwenye chati na kukupa heshima kubwa sana. Nyimbo Ambazo mwanzo hukuzielewa lakini baada ya kuziachia zimekuwa Ndo nyimbo zako pekee kali zinazotamba hadi hii leo. Nilikukaribisha nyumbani kwangu, hata kudiriki kuwahamisha baadhi ya Watu ili wewe upate chumba cha kujisitiri. Na hata ulipoamua kuhama sio kwamba nilikufukuza,” aliongeza.

“Ulitamani uhuru wa kukaa peke yako ili uweze kufanya Yale uyapendayo. Na hata ulivyoamua hivyo bado nilikujali, na kukilipia kodi chumba kipya ulichokipata. Mara nyingi ulisanda na kutamani kurudi nyumbani, ahadi yangu ikabaki palepale kwamba kwangu Ni nyumbani kwako. Ulikuja mara nyingi japo kula chakula. Mara ya Mwisho nakumbuka kodi niliyokulipia iliisha, ukakosa pa kuishi watu wakakuita Yahaya. Popote usiku mnene ulipokukuta ndipo ulipoangusha, hukuona tena umuhimu hata wa kutafuta kwako.”

“Ulevi ukaendeleza tena uliopindukia, habari zikaanza enea kwamba unabuya unga. Hayo uliyakana kwa nguvu zako zote, lakini popote ulipoonekana watu walinukuu. Kwa Upendo tulikuita uvumi kuuchunguza, yetu ukayapuuza na kufanya yaliyo yako. Inaniuma hadi mtimani, kuona unapotea, lakini Mola ajua Ni Mara ngapi nimejaribu.”

Kwenye maelezo mengine, Millian amesema, “Ni Nani utakayemlaumu kwa umasikini wako? Ni nani aliyekwambia uyaache yaliyo ya maendeleo na kujiingiza kwenye magenge ya wahuni? Kama usiposhtuka sasa hivi na kugundua kuwa huna hata chumba cha kupanga au hata begi la nguo Halafu unajiita Msanii wa muziki utastuka when it’s very late. Washkaji zako wote ni wahuni, bangi, cocaine, pombe na madem wasiojua hata kuandika aeiou. Hayo sio maisha! Nimekuonyesha njia ukaniona bwege. I am not responsible for your downfall. And if you don’t know, you’re about to hit rock bottom. Get up before we lose another very potential artist.”

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment