Katibu mkuu wa BASATA, Godfey Mngereza akiwa na Diamond kwenye mapokezi yake baada ya kutoka Marekani, Alhamis hii
Akizungumza na Bongo5 jana, katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza ,
alisema moja ya vitu vinavyosababisha kutoelewana na wasanii ni
mashabiki.
“Kutoelewana (Diamond na Alikiba) ni kitu ambacho kinanisikitisha
sana,” alisema. “Kwa sababu moja mkiwa kwenye tasnia moja mnatakiwa
kuangalia jinsi ya kusonga mbele kwa tasnia pamoja na mafanikio ya mmoja
mmoja. Ndio maana nikasema huu ushabiki sio mzuri sana. Inatakiwa kuwe
na ushabiki wa kujenga,” aliongeza.
“Pia watambue mashabiki wao wanaweza kujenga au kubomoa. Lakini kwa
sasa kitu kinachosababisha kutokea sintofahamu ni professionalism. Kwa
sababu mtu anaweza akazingatia ushabiki kumbe hauendani na weledi.
Kwahiyo wasanii waangalie ushabiki unaweza ukakujenga au ukakubomoa kwa
njia moja au nyingine. Ndio maana tunasema ukipata sifa usilewe sana,”
alisisitiza Mngereza .
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment