Abby na Ommy Dimpoz
Ommy Dimpoz pia amechukua uamuzi wa kumuongeza mtangazaji wa Choice
Fm, Abby Plaatjes kwenye management yake, ambaye sasa ataungana na
meneja wake wa toka mwanzo Mubenga.
“kwenye management kumeongezeka mtu tunafanya kazi na Abby wa Choice
Fm, she is my manager anasaidiana na Mubenga, unajua Mubenga ni mtu
ambaye nimekuwa nae from day 1,” Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5.
Staa huyo wa ‘Wanjera’ ambaye ameibuka na tuzo ya AFRIMMA 2015 ‘Best
Newcomer’ weekend iliyopita huko Marekani, amesema kuwa Abby ataleta
mchango hasa kwa soko la kimataifa kutokana na uzoefu na connection
zake.
“Kwa Abby naye ana uzoefu tofauti, ana connections tofauti amekuja
kusaidia kazi kikubwa zaidi tunatakiwa kumove kutoka hapa tulipo
kuelekea sehemu nyingine, wenzetu wanaweza wakawa na mameneja hata
kumi lakini kutokana na aina yetu ya soko jinsi lilivyo unajitahidi pale
unapoweza.”
Abby amewahi kufanya kazi pia na Vanessa Mdee pamoja na Linah Sanga kama meneja.
Kutokana na kuongeza meneja kuna mambo ambayo Ommy amewaahidi mashabiki kuona utofauti kuanzia sasa.
“So far tunafanya kazi na Abby kuna mambo mengine makubwa yatakuja na
watu wataona kwamba kweli sasa hivi kuna mabadiliko kuanzia kiuongozi
mpaka kazi za Ommy Dimpoz, unajua tunaelekea kwenye mwaka mpya kwahiyo
lazima tuje na mambo mapya.”
Ommy ameongeza kuwa miongoni mwa maboresho mengine ya kiuongozi
ambayo wameyafanya kwa sasa pia wana mwanasheria rasmi atakayekuwa
akihusika na mambo ya kisheria ya Ommy Dimpoz na PKP.
Kwenye safari ya Dallas, Marekani kwenye tuzo za AFRIMMA Ommy
aliambatana na mameneja wake wote wawili Mubenga na Abby, pamoja na
dancers wake kitu ambacho hapo awali alikuwa hafanyi, kusafiri na watu
wengi kwenye shughuli zake za kimuziki.
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment