Kwenye mahojiano aliyofanya na Jarida la ‘New York Times’ Nick amesema “Siipendi, inanifanya nijisikie vibaya. Haitakiwi kuchagua upande wowote kwa watu unaowapenda, Ni ujinga. nataka tu iishe”
Pia ameongelea kuhusu kumpa Miley Cyrus makavu yake baada ya kushinda tuzo wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo za ‘MTV VMA’ Nick Minaj amesema
“Inashangaza mtu anaponifikilia vibaya kwasababu nimeongelea
vitu vinavyowaathiri wanawake weusi, inanifanya nikuone una matatizo
yako binafsi” Aliongeza “Kwenye video zako
unatumia wanaume weusi, stejini unapanda na wanawake weusi, lakini
hutaki kujua wanawake weusi wanajisikiaje kuhusiana na vitu vya muhimu
kwenye maisha yao? Hapana, huwezi kutaka vitu vizuri tu, kama unataka
kufurahia tamaduni zetu na aina ya maisha yetu, kaa karibu yetu, cheza
na sisi, furahi na sisi, imba na sisi lakini lazima ujue matatizo yetu,
nini kinatusumbua, kipi tunaona hatujatendewa haki, lakini cha
kushangaza hutaki kujua”
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment