Monday, 12 October 2015

Diamond, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz washinda tuzo za Afrimma

Diamond Platnumz ameibuka na ushindi mkubwa zaidi kwenye tuzo za Afrimma zilizofanyika Dallas, Marekani alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu; Best Dance Video ya wimbo wake Nana, Best Male East Africa na Artiste Of The Year.

“EA well represented at the #Afrimma2015 & The Best Winner of the night goes to @diamondplatnumz with 3 Awards!! Salute all EA,” ameandika mtangazaji wa Citizen TV/Radio Citizen, Willy M Tuva aliyekuwepo kwenye tuzo hizo.

Pia wimbo alioshirikishwa na kundi la Bracket, Alive umeshinda tuzo ya Best Inspirational Song.

 
Vanessa Mdee ameshinda tuzo ya Best Female East Africa. “Asante Asante Sana. You believed in me. Thank you,” ameandika kwenye Instagram. Naye Ommy Dimpoz ameshinda tuzo ya Best New Comer.

Washindi wengine ni pamoja na..
Godfather (Best Video Director), 
AKA (Best Male South Africa, Best Collabo), 
Yemi Alade (Best Female West Africa), 
Davido (Best Male West Africa), 
Wizkid (Video of the Year, Ojuelegba), 
Yuri (Best Male Central Africa).  

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment