Msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri na Track yake ya ‘Ligi ndogo’Billnas amesema kipindi cha uchaguzi ndio kiupindi kizuri zaidi kuachia kazi mpya tofauti na wasanii wengi wanavyofanya kwa madai ya kuwa kipindi hiki cha siasa watazamaji wa runinga na wasikilizaji wa redio wanaongezeka.
Akiongea na kipindi cha XXL cha CloudsFm, Billnas amesema
“TUnatofautiana kuamini, mimi naamini kwenye msimu wa siasa ndio
usikilizaji wa redio unaongezeka alafu ata uangaliaji wa Televisheni,
kuna watu wengi labda walikua wanaangalia televisheni za nje ya nchi
lakini ikifika kipindi ichi ndio wanaangalia local channels kwasababu ya
mambo ya kisiasa wajue taratibu nzima za nchi yetu zinavyoenda
hususani kipindi hiki cha siasa, unakuta labda wakati mtu anasuburi
aangalie taarifa ya habari anaweza akakutana ligi ndogo inapigwa..
kwahiyo naamini usikilizaji umeongezeka..”
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment