MKALI wa R&B nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’ ameweka wazi sababu za
kuitwa kwenye msimu mpya na wa tatu wa Coke Studio uliofanyika nchini
Kenya wiki kadhaa zilizopita kuwa ustaa ulichangia kuitwa kwake.
Akizungumza na Risasi Vibes, Ben Pol anayetamba na Wimbo wa Sophia
alisema kuwa, hakuwa anajua kama atashiriki msimu huu mpya, lakini
alishangaa kupigiwa simu na Coke Studio kisha kuambiwa atakuwa mmoja
wapo atakayeiwakilisha Bongo na walifanya hivyo baada ya kumfuatilia
kazi zake mitandaoni hususan Mtandao wa Youtube.
“Kwa kiasi kikubwa ustaa wangu umenifanya nishiriki katika msimu huu
mpya wa Coke Studio. Namshukuru Mungu muziki wangu kukubalika kila pande
kumenifanya nionekane nje ya Tanzania,” alisema Ben Pol.
Msimu mpya wa Coke Studio utaanza kuonekana kwenye TV mbalimbali nchini
kuanzia Oktoba 10, mwaka huu huku staa huyo akiwa amefanya ngoma kibao
na staa wa muziki nchini Kenya, Wangechi kama vile Sophia, Ningefanyaje
na Jikubali.
Ingia hapa ili ku-download NINGEFANYAJE YA BEN POL
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment