Licha ya kukithiri kwa tatizo la wizi wa kazi za sanaa Tanzania, kundi la muziki la Weusi lina mpango wa kuuza album yao kwa njia ya watu kudownload mtandaoni.
Msemaji wa kundi hilo, rapper Nikki Wa Pili amesema kuwa wanaamini
kwamba hiyo ni njia itakayowapunguza nguvu maharamia wa kazi za wasanii.
“Plan yetu ni kuweka kwa njia kama ya Mkito, na sisi tulikuwa
tunajaribu kuongea na jamaa kama wa Mkito tunaweza tukatoa album yetu
kule then watu waka-download. Tunafikiria kwa namna hiyo angalau watu
watajua album ya Weusi inapatikana lakini kwa njia ya kudownload kwahiyo
hapo itakuwa imetoa information ambayo itamkwepesha huyu pirate na vile
ambavyo tunatangaza. ..tunaona njia safe ni kuuza kupitia watu
kudownload.” Alisema Nikki Wa Pili kupitia 255 ya Clouds Fm.
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment