Thursday, 9 July 2015

‘Nchi ya Ahadi’ yampa shavu Kala Jeremiah kufanya kampeni ya kuhamasiha Watanzania kupiga kura

Kala Jeremiah amesema kuwa wimbo wake ‘Nchi ya Ahadi’ aliomshirikisha Roma umempa shavu la kufanya kampeni ya kuhamasisha watanzania kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Kala ameiambi Bongo5 kuwa atazunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kutoa elimu kwa watanzania kuhusu kutumia vitambulisho vyao vya kupigia kura kuchagua viongozi wanaowataka.

“Kabla wimbo haujatoka tulikuwa na mawazo ya kuingiza maneno ya kuhamasisha watu kupiga kura lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kufanya hivyo. Lakini baada ya kutoka wimbo pamoja na video na kusambaa, Mungu sio athumani kuna tasisi imenifuata ina idea ya kuhamasisha watu,” amesema.



“Kwahiyo automatic kwa kupitia ule wimbo, wakaona nilichokiimba kinafaa kuwa kwenye harakati zao za kuhamasisha jamii kuhusu watu kujitokeza kwenye kupiga kura baada ya kuona kuna baadhi ya watu wamejiandikisha ili wapate vitambulisho kwa matumizi yao binafsi na si kupiga kura. Sasa sisi tutaingia kati yao na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa kura yao hata kama kutakuwa na jua kali au mvua. Kwahiyo hiyo ndio deal iliyoingia kupitia Nchi ya Ahadi.”

-Bongo 5

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment