Thursday, 9 July 2015

Haya ndio masharti aliyotoa Diamond Platnumz kwa Msanii wa Tanzania anaetaka Collabo nae.


Muimbaji huyo wa ‘Nana’ ameyasema hayo baada ya kuulizwa kwanini hafanyi collabo nyingi na wasanii wa Tanzania.

“Mimi sina tatizo as long as nijue hiyo kazi unayotaka kufanya na mimi itafika wapi,” alisema Diamond kupitia Clouds E.

“umejipanga vipi project yako na umeiandaa vipi, kwasababu sitaki nifanye tu nyimbo mwisho wa siku halafu iishie tu ndani unaiskiliza wakati natumia muda kukaa kuandika kupoteza muda studio.“

Aliendelea kwa kujitolea mfano yeye anapofanya collabo na msanii wa nje, lengo kubwa huwa ni kujitangaza zaidi kule anakotoka msanii anayemshirikisha.

“Na ukiangalia kwa mfano kama nje nakuwa nafanya collabo na wasanii tofauti tofauti kwasababu inasaidia pia muziki wetu kutanua kiurahisi[…] Lakini haimaanishi kwamba sitaki kufanya collabo na wasanii wa Tanzania […] yaani unavyokuja kufanya collabo lazima ufanye kuonesha qualification za kufanya tufanye collabo.”

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

No comments:

Post a Comment