Friday 30 June 2017

Tetesi za usajili soka Ulaya Ijumaa Juni 30. 2017



Manchester City sasa wanaongoza katika mbio za kumsajili Alexis Sanchez, 28, baada ya Bayern Munich kujitoa kutokana na bei kubwa ya mchezaji huyo wa Arsenal (Daily Mirror).

Manchester City wana uhakika wa kumsajili Alexis Sanchez kwa takriban pauni milioni 50, kwa sababu ya hamu ya mchezaji huyo kufunzwa na Pep Guardiola (Guardian)

Chelsea wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris St-Germain katika kumsajili beki Alex Sandro, 26, huku Juventus wakitaka pauni milioni 61 (Daily Mail).

Chelsea wanatazamiwa kukamilisha usajili rasmi wa Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco wiki hii (The Sun).

Wakala wa kiungo wa Chelsea Mario Pasalic, wamekutana na Real Betis kujadili uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Spain (Marca).

Manchester United watazidiwa kete na Paris St-Germain katika kumsajili kiungo kutoka Brazil, Fabinho, 23 anayechezea Monaco (Daily Record).

Dau la Arsenal la zaidi ya pauni milioni 30, la kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar, 21, limekataliwa, na sasa Arsenal wanafikiria kukamilisha usajili wa Riyad Mahrez, 26, kutoka Leicester (Telegraph).

Barcelona, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomnyatia winga wa Monaco, Thomas Leimar (L”Equipe).

Arsenal wanamtaka kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 25, baada ya Roma kukatishwa tama na bei ya pauni milioni 35 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast (The Sun)

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud anakaribia kurejea Ufaransa, huku Lyon na Marseille wakimtaka, na Arsenal ikitafuta mtu wa kuziba pengo lake (L’Equipe).

Chelsea huenda wakatibua dau la Zenith St Petersburg la pauni milioni 26 la kumtaka beki wa Roma, Kostas Minolas, huku mchezaji huyo pia akisita kuhamia Urusi (Daily Telegraph).

Michel Keane hatarajiwi kurejea Burnley kwa sababu Everton wanatarajiwa ‘kulazimisha’ usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii (Burnley Express).

Michael Keane atagharimu pauni milioni 25 (Times).

Mshambuliaji wa Watford Stefano Okaka, 27, amepewa dau kubwa la kuhamia Shanghai Shenhua ya China (The Sun).

No comments:

Post a Comment