Thursday 29 June 2017

Diamond akiri kuwafungia vioo mademu WCB


Kiongozi wa lebo ya WCB, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, amesema kumsajili msanii wa kike katika lebo hiyo ni mtihani mkubwa, kutokana na jinsia hiyo kuwa na changamoto nyingi.

Kauli ya Diamond imekuja baada ya hivi karibuni kuwasajili katika kundi la Wasafi wasanii Mr. Lavalava na Maromboso, ambao kwa sasa wanafanya kazi chini ya lebo hiyo.

“Ukweli kumsajili mtoto wa kike ndani ya lebo yetu ni mtihani, siyo kwamba nawatenga, hapana na ninaomba watu wasinielewe hivyo, kifupi tu watoto wa kike wana mambo mengi, mfano akiolewa huwezi kumpata kirahisi kwenye majukumu ya kazi na mengineyo,” alisema Diamond.

Diamond alisema moja ya masharti ndani ya lebo hiyo ni pamoja na kuwasajili wasanii wenye uwezo mdogo kimaisha, pia ametaka wajifunge ili waweze kufanya kazi kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment