Thursday 29 June 2017

RayVanny mbioni kufungua studio


Msanii kutoka Wasafi Classic, Raymond, maarufu kama Ray Vanny, anatarajia kufungua studio yake ya kurekodi muziki, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utendaji wa kazi zake na kujitanua kiuchumi.

Kwa mujibu wa kiongozi wa lebo ya Wasafi, Nassibu Abdul,’Diamond Platnumz’, wamempa baraka zote msanii huyo kwa kupiga hatua hiyo kubwa ya kimaendeleo.

“Ni kweli Ray Vanny yupo kwenye maandalizi ya kufungua studio yake na mimi kama kiongozi wa kundi nimefurahishwa na ndoto za msanii huyo, kwani ni hatua kubwa katika maisha ya muziki,” alisema Diamond.

Aliongeza, “Ni jambo la mafanikio kuona wasanii ambao nimewasaidia wakifanya mambo makubwa kama haya, nadhani ni wakati mwafaka wa kuwapa sapoti,”.

No comments:

Post a Comment