Mpira sasa ni biashara, wenzetu walioendelea hawazingatii tu matokeo ya ndani ya uwanja bali nje ya uwanja pia ni suala kubwa linaloangaliwa sana na vilabu vya wenzetu hasa katika masuala ya masoko.
Kati ya vitu muhimu katika kujitangaza kibiashara ni mitandao ya kijamii, na ukizungumzia mitandao ya kijamii huwezi kuiacha Facebook ambao ni kama mtandao mama kwa hii mitandao ya kisasa. Real Madrid wameipiga Barcelona bao katika Facebook, kwa muda mrefu Barcelona wamekuwa wakiongoza kuwa klabu yenye mashabiki wengi Facebook ikiwa na idadi ya watu mililioni 100.
Lakini sasa Real Madrid wamekaa juu ya Barcelona kwani Madrid sasa ana mashabiki milioni 100.46 huku Barcelona wakiongezeka hadi milioni 100.02, na hivyo Barca kuwa wapili chini ya Madrid.
Manchester United ni klabu ambayo yenyewe huwa ukitaja miamba hii miwili ya Hispania kuhusu ukubwa na uwezo baasi jina la United lazima litokee katikati yao, juu yao au chini yao na hapa katika orodha hii United wako nafasi ya 3 na wafuasi milioni 73.
Chelsea wako nafasi ya nne na ongezeko lao la mashabiki mitandaoni linakuwa kwa kasi sana kwani hadi sasa Facebook wana wafuasi milioni 47 huku Bayern Munich akiwa na wafuasi milioni 41. Arsenal wako nafasi ya 6 na wafuasi wao milioni 37 huku Liverpool wenye wafuasi milioni 31 wakiwa nafasi ya 7 na miamba ya Ufaransa PSG nafasi ya 8 wakiwa na wafuasi milioni 27.
Miamba miwili ya Serie A Juventus na Ac Millan wanafunga orodha ya timu 10 zenye wafuasi wengi
Facebook, Juventus wakiwa wa 9 na wafuasi 25 milioni ikiwa ni wafuasi milioni 1 zaidi ya Ac Millan walioko nafasi ya 10 na 24 milioni.
No comments:
Post a Comment