Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) akana kutoa taarifa za ndoa yake.
Hivi karibuni magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yaliobnekana kufanya
mahojiano na mrembo huyo na kuripoti kuwa ndoa yake na mpenzi wake
Fransic Shiza maarufu kama Majay ambaye pia ni bosi wa EFM na TVE
inakaribia.
Kupitia mtandao wa Twitter, Lulu amekanusha taarifa hizo kwa
kuandika, “Hivi kwa Akili yenu Ndoa inatangazwaga Kwenye
Magazeti!??Muwege mnajiongeza kabla ya kuparamia Story…!.”
Kwenye gazeti la Mtanzania la siku chache zilizopita, lilinukuu kauli
ya muigizaji huyo aliyosema, “Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa
yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane
wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni.”
No comments:
Post a Comment