Msanii wa muziki wa pop nchini Marekani, Janet Jackson (50), ameweka
wazi kwamba kwa sasa yupo huru kufanya mambo yake na anajiandaa kurudi
kwenye kazi yake ya muziki baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake,
Wissam Al Mana, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msanii huyo ameonekana juzi kwa mara ya kwanza akiwa na mtoto wake
ambaye hajawahi kuonekana tangu alipozaliwa miezi mitatu iliyopita.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Janeth aliandika kwamba, baada ya
kuachana na mume wake huyo yupo huru kufanya mambo yake ikiwamo muziki
ambao anadai wakati akiishi na mwanamume huyo hakutaka afanye muziki.
“Muda mfupi ujao nitaanza kuendelea na harakati zangu kama awali,
nilikuwa kwenye ndoa nikawa nashindwa kufanya baadhi ya mambo, lakini
kwa sasa nipo huru nikimlea mwanangu na muda mfupi nitarudi kwenye kazi
yangu ya muziki iliyonipatia fedha na jina kubwa,’’ alisema Janet.
No comments:
Post a Comment