Msanii wa muziki wa Pop nchini Marekani,, mwenye miaka 50, anatarajia
kuingiza kiasi kikubwa cha fedha baada ya kuachana na mume wake tajiri
kutoka Qatar, Wissam Al Mana.
Janet amethibitisha kuachana na mume huyo kwa madai kwamba, tajiri huyo
hana mapenzi ya dhati na amekuwa akiibagua familia yake.
Wissam Al Mana ni mfanyabiashara mkubwa duniani anayemiliki kampuni
kubwa zaidi ya 55, kuvunjika kwa ndoa yake kunadaiwa kutampa utajiri
mkubwa Janet, atakayekuwa kimlea mtoto wao mmoja wa kiume aliyezaliwa
Januari, mwaka huu.
Wissam Al Mana anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya pauni milioni 800, zaidi ya Sh trilioni mbili za Tanzania. Hata hivyo, sheria za Marekani ni kwamba wanandoa wakiachana wanatakiwa
kugawana mali, hivyo kutokana na hali hiyo, Janet anaweza kupata zaidi
ya Sh trilioni moja, ikiwa ni sehemu ya mgawo wa kuachana kwao pamoja na
kiasi kingine cha huduma kwa mtoto wao.
Kitendo hicho ndicho kinachowafanya wasanii matajiri nchini Marekani
kuchelewa kufanya maamuzi ya kufunga ndoa, wakiogopa kugawana mali
watakapoachana.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Janet inaeleza kwamba, msanii huyo
alilenga kudumu kwenye ndoa kutokana na umri wake mkubwa na hakufuata
fedha kwa kuwa naye ana utajiri wa zaidi ya dola milioni 150 za
Marekani, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 331 za Tanzania.
No comments:
Post a Comment