Tuesday 28 March 2017

Nikki wa Pili awapa darasa BASATA


Msanii Nikki wa Pili kutoka katika kampuni ya Weusi amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufanya mpango kuwaita wasanii kwa ujumla ili wakae pamoja waweze kuwaweka sawa juu ya neno "maadili" linalotumiwa kama fimbo ya kuwachapa 'wasanii'. 

Ametoa neno hilo jana wakati wakitambulisha wimbo wao mpya unaoitwa 'Ya Kulevya' kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio amesema wamekuwa katika njia panda baada ya kushindwa kuelewa neno hilo linavyotumika huku akiwatoa wasiwasi wadau wa muziki na mashabiki zao kuwa wimbo huo mpya hauna maana ya vitu vinavyoendelea nchini kwasasa.

"Wimbo wetu wa 'Ya kulevya' huu ni wimbo wa mapenzi unaozungumza juu ya mwanaume aliyependwa sana na mkewe na familia yake, upendo ukamlevya akaanza kujisahau na kula bata na mwishowe kuharibu familia, tunasikitishwa na watu wanaojaribu kubadili maana hii, imekuwa kawaida kwa msanii kutumia maneno au misemo iliyoko katika jamii wakati huo kwani hata matangazo ya biashara, 'Comedy' hufanya hivyo ili kuwavutia wateja wao". Alisema Nikki wa Pili

Vile vile msanii huyo alisisitiza kwa kusema kuwa kabla ya kutoa kazi hiyo imekaguliwa na chombo cha maudhui ya sanaa

No comments:

Post a Comment