Kiungo mshambuliaji kutoka timu ya Taifa Stars, Saimon Msuva amesema
mechi inayotarajiwa kuchezwa leo dhidi ya Burundi itakuwa
kali zaidi kwa sababu wanataka kufuta historia ya kufungwa na timu hiyo.
Mshambuliaji huyo amesema walikuwa
hawajuani vizuri na kikosi hicho ndiyo maana ilipelekea wao kuwekwa
katika rekodi ya kufungwa mara zote mbili walipokutana nao.
“Unajua Burundi tumecheza
nao mara mbili na zote wametufunga, kwa hiyo tunataka tulipize kisasi,
Hawa Botswana tulikuwa tunacheza nao hatujuani vizuri, lakini Burundi
tunajuana sana kwa hiyo mechi itakuwa ngumu sana,” Alisema Msuva
Pamoja na hayo kiungo huyo alionesha
hali ya wasiwasi juu ya mchezaji Laudit Mavugo kutokana na uzuri wake na
kusema atawasumbua katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment