Mkongwe wa bongo fleva Juma Kassim Nature 'Sir Nature' amekanusha vikali
kulipwa na msanii Harmorapa katika wimbo wa 'Kiboko ya mabishoo' na
kudai kwamba kijana huyo hana pesa za kumlipa na kusisitiza yeye
alifanya kwa upendo tu.
Nature amesema kwamba alikubali kushiriki katika wimbo huo kwa sababu
anaamini msanii huyo chipukizi ana uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na
kuamini atafika mbali.
"Nikisema nimemlipisha
Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea, mimi ni mtu mzima
nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua
muziki pia na imani atafika mbali, hawezi kunilipa mimi, ana hela gani". Alisema Juma Nature ndani ya EATV.
Katika hatua nyingine Nature kutoka TMK
amesema yeye ameshakuwa mkongwe hivyo vijana kama kina Harmorapa
wanapotokea kwenye ‘game’ inamlazimu kutoa sapoti ili hata
watakapoondoka kuwe na watu wa kuendeleza muziki.
Aidha Nature amekanusha kusikia taarifa
ambazo Harmorapa alidai kuwa amemlipa Nature kwa kolabo na kuongeza hizo
taarifa kwa upande wake hazimkufikia rasmi.
Hata hivyo Harmorapa aliwahi kunukuliwa
akisema siyo busara kwa wasanii wakongwe kuwalipisha pesa wasanii
wachanga kwa kuwa ndiyo kwanza wanaanza kutafuta pa kutokea na kuweka
wazi kuwa kwa upande wake alilazimika kumnunulia nguo Nature za kufanyia
video ya ‘Kiboko ya Mabishoo’.
No comments:
Post a Comment