Klabu ya Manchester City imetozwa faini ya Pauni 35,000, baada ya kukutwa na hatia ya kushindwa kuwazuia wachezaji wake wasifanye vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wa ligi ya England dhidi ya Liverpool uliochezwa Machi 20.
Chama cha soka nchini England kiliifungulia mshataka klabu hiyo ya
mjini Manchester baada ya kufuatialia kwa kina matukio kadhaa ya utovu
wa nidhamu yaliyoonyeshwa na wachezaji wa Man City, na kubwa zaidi
lililopewa uzito ni lile la kumzonga mwamuzi Michael oliver katika
dakika 50 alipoamuiru mkwaju wa penati uliosababishwa na beki wa pembeni
Gael Clichy kwa kumchezea ndivyo sivyo mshambuliaji Roberto Firmino.
Katika tukio la kumzonga mwamuzi, kiungo mshambuliaji wa Man City David Silva alionyeshwa kadi ya njano. “Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu, tumebaini Man City walikuwa na
hatia ya utovu wa nidhamu wakati wa mchezo dhidi ya Liverpool na benchi
la ufundi lilishindwa kusimamia kitendo hicho kisitokee, hivyo tunaitoza
faini ya Pauni 35,000.” Ilieleza taarifa ya FA.
Man City wamekumbwa na adhabu hiyo, wakiwa katika mipango ya kusafiri
hadi jijini London, kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu mwishoni mwa juma
hili ambapo watacheza dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.
No comments:
Post a Comment