Tuesday 26 April 2016

Video | Raymond Asimulia Jinsi Alivyomshawishi Diamond Hadi Kumchukua WCB


Raymond amesimulia jinsi ambavyo alimshawishi Diamond hadi kuamua kumchukua kwenye label yake, WCB.

Ameiambia Bongo5 kuwa alipigiwa simu na mshkaji wake, Maromboso aende studio kuungana naye katika kusikiliza wimbo wa Diamond aliokuwa anataka mawazo ya watu wengi.

“Brother Diamond akifanya ngoma anapenda management yake, kuanzia madancer, mameneja wote waweze kusikiliza wimbo wake. Katika hiyo crew ya watu waliokuwepo Maromboso akapendekeza na mimi niwepo,” amesema.

Anasema baada ya kumshauri vitu kadhaa Diamond aligundua ana kitu cha ziada na kumuuliza kisa cha kutotoka hadi muda huo. Amedai kuwa Diamond alimuomba nyimbo zake azisikie na akawa anamshauri vitu vya kurekebisha. Aliendelea kurekodi nyimbo kwenye studio mbalimbali na kuwa anamtumia hadi alipofungua studio ya WCB.

Anasema kuwa kwenye studio hiyo alirekodi nyimbo nyingi kali zilimchanganya Diamond na uongozi wake hadi wakashindwa watoi upi.

Ray ameongeza kuwa Bado ilitoka kwa mbinde kwakuwa kulikuwa na nyimbo zingine kali sana. Mtazame hapo chini kumsikia akielezea.



Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment