Muimbaji huyo wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, atakuwa chini ya
usimamizi wa Said Fella. Ferooz amesema wimbo huo unaongelea mambo
magumu aliyoyapitia wakati alipokuwa kwenye matatizo na jinsi watu
aliowategemea kuwa naye walivyomkimbia.
“Nimejifunza vingi, nilikuwa nipo kimya, nimeexperience mambo mengi,
unajua unapokuwa upo kimya, unapokuwa kwenye matatizo, unapokuwa haupo
juu yaani unapokuwa haupo kazini unakutana na changamoto nyingi,”
ameiambia Bongo5.
“Wazuri wako utawajua na wabaya wako utawajua. Ukisikia wimbo ndio
utajua mambo mengi zaidi lakini nimejifunza vitu vingi kutokana na
maisha yangu na vitu nilivyopitia hapa katikati.”
Ferooz amesema ameamua kuwa chini ya Mkubwa Fella kwasababu ni mtu
ambaye amekuwa akimsupport kwa muda mrefu, hajawahi kumuangusha na ana
uelewa mzuri kuhusu tasnia ya muziki.
Kwa upande wake Fella ameiambia Bongo5 kuwa aliwahi kumsimamia Ferooz
miaka kadhaa iliyopita kipindi ameachia wimbo ‘Ndege Mtini’ na
kumrudisha kwenye chati lakini marafiki ‘feki’ walimshauri ‘ujinga’ na
kumpoteza tena.
“Mimi niliona isije Ferooz akala unga tukaanza kusaidia kwenye kula
unga. Nimemuita nimekaa naye chini nikamuambia ‘mwanangu sikiliza
inabidi sasa twende vile ninavyotaka mimi, cha msingi haya ni maisha
yako, ukitegemea marafiki wanakuja wanakuzingua unaenda nao mnaachana
ukiwa na maisha magumu unakuja kwangu tena’ basi tukakubaliana na hata
nyimbo yenyewe nimeiandika mimi kasema kabisa tunaandika nyimbo inaitwa
Nimejifunza. Ukiwa na maisha mazuri huwezi kujua rafiki mbaya, ila
ukichoka unajua rafiki mbaya,” amesema Fella.
-Bongo5
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment