Saturday, 24 October 2015

Weusi wataja sababu za kutofanya show za kampeni za kisiasa, Wataka Watanzania wapige kura kwa amani

Kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Nikki wa Pili, G Nako jana walikuwepo kwenye show ya Friday Night Live ya EATV ambapo walizungumza kuhusiana na sababu zilizo wapelekea kutofanya show za kisiasa kipindi cha kampeni na kuwasihi Watanzania wapige kura kwa amani.

Wasanii hawa walifafanua kuwa wao wanatangaza amani hivyo haikuwapasa wao kuingia kwenye kampeni za kisiasa kwa chama chochote kile ili kukiunga mkono kushinda katika uchaguzi mkuu wa 24th Oct, 2015 bali Watanzania kuchagua chama chochote ambacho watakacho kipenda.

Nikki wa Pili alisema kuwa "Watanzania hawana hofu na uchaguzi, Bali wanao gombea uongozi ndio wana hofu na uchaguzi", Nikki amewataka Watanzania kutoingia kwenye hofu hiyo ya viongozi kwa kufanya vurugu kuwatafutia maisha hao viongozi.

Naye Joh Makini na G Nako walikuwa na usemi mmoja kuwa utakapo pambana kwaajili ya kufanya kiongozi uliye mchagua ashinde hautakuwa ukitafuta masha yako bali utakuwa unapambana kwaajili ya maisha ya mtu mwingine na sio yako wala ya familia yako.

Mbali na kuzungumzia uchaguzi kwa amani, Weusi wanatarajia kuachilia baadhi ya kazi zao kwanzia juma lijalo ikiwa ni Nikki wa Pili kuachilia ngoma yake mpya yenye vionjo vipya tofauti na vilivyo zoeleka, Kisha Joh Makini na G Warawara kuachilia video zao walizo zifanya Afrika Kusini.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment