Harmonize licha ya kuwa ni msanii mpya lakini safari yake ya kimuziki
imeanzia kwenye matawi ya juu ambayo kuna baadhi ya wasanii wakubwa
hawajawahi kuyafikia.
Harmonize amesema kuwa video ya single yake ya kwanza ‘Aiyola’ tayari
imekamilika, ikiwa imeshootiwa Afrika Kusini na director aliyeongoza
video ya mastaa wa Nigeria, ‘Dorro bucci’ pamoja na ‘Love Boat’ ya Kcee
na Diamond.
Kupitia Planet Bongo ya EA Radio, Harmonize ameongeza kuwa tayari
amewasiliana na director na amemtumia video hiyo ikiwa imekamilika.
Sina shaka siku si nyingi tutaanza kumuona Harmonize akisumbua kwenye
vituo mbalimbali vya kimataifa kama Trace na MTV Base ambavyo vimekuwa
ni ndoto za wasanii wengi wa Bongo.
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment