Friday, 16 October 2015

Video mpya ya Vanessa Mdee ‘Never Ever’ imegharimu kiasi hiki


Mbali na hayo siku hizi biashara ya muzkiki sio idadi ya show tu bali hata utengenezaji wa video nzuri nayo ni sehemu muhimu sana kwenye kutengeneza muziki mzuri, video nzuri hutoa nafasi ya wimbo wa msanii kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV, Africa pia huchangia kwa kiasi kikubwa kumpeleka msanii kwenye majukwaa mbalimbali ya kuwania tuzo mbalimbali.



Je, unajua Vee Money katumia kiasi gani cha pesa kutengeneza video yake mpya!? 
Inawezekana imekufikia au haijakufikia, lakini kama ilikupita ichukue hii… Vanessa Mdee amesema kwamba video yake mpya ‘Never Ever’ imetumia zaidi ya dola 20,000 kuifanikisha kwenye ubora wake, ambayo kwa pesa ya nyumbani tunazungumzia kiasi cha Tzs. Milion 40!

money2 

Kwa mujibu wa mtandao wa CloudsFM Vanessa Mdee alizungumza kuhusu video yake mpya ambapo pia alisema…
>>> “Video ya wimbo wangu wa Never Ever imenigharimu dolla elfu 20 sawa na Mill. 40 za Kitanzania nimefanya kwa producer Justin Compos, na malengo yangu bado sana hata sijafika ukurasa wa pili wa kitabu ninachoandika na matumaini ya kuvuka mipaka mingi zaidi…’<<< Vanessa Mdee.

Ku-download ngoma hii Ingia Hapa

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment