Kuongea hakikuwa kitu kigumu kwa muimbaji huyo wa Nana, bali lugha aliyotakiwa kutumia – Kiingereza, ilikuwa inampita kushoto wakati huo.
“Wakati naanza shughuli za muziki, nasema sasa nataka kwenda international, lilikuwa ni suala gumu sana,” Diamond alisema wakati akihutubia kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule ya Righway ya Dar es Salaam alikoalikwa kama mgeni mashuhuri Jumapili, Oct 18.
“Nakumbuka mara ya kwanza nimeenda Big Brother kuperform, Tale
ananiambia ukishamaliza kuperform utaulizwa maswali. Mimi nikamwambia
meneja wangu Babutale, yale maswali yataulizwa live pale, nitazungumza
nini? Ilikuwa mtihani. Cha kujibu ilibidi niambiwe nikikariri kwanza
ili nikiweke kwenye kichwa, ilikuwa kazi kubwa sana,” alisimulia
Diamond.
“Nikajiuliza nikasema, mimi nataka kwenda international muziki wetu
wa Tanzania, Bongo Flava ufike mbali, sasa ntaufikisha vipi ikiwa lugha
[Kiingereza] mgogoro? Palikuwa na kazi hapo! Kila nikijaribu kubabaisha
naona hapana, akili inaniambia Diamond unatakiwa utafute mwalimu.”
“Nikasema I need to go back to school, nikajifunze. Wakati natoa hilo
wazo kwa baadhi ya watu na wasanii wenzangu wakawa wananicheka wanasema
elimu ya ukubwani, walikuwa wananicheka sana. Nikasema kila mtu na
mipango yake, niachane na mipango yangu, nikawa namuita mwalimu
ananifundisha pale japokuwa ratiba yangu ilikuwa inabana nasafiri sana
lakini napopata muda najifunza,” aliongeza.
“Namshuru mwenyezi Mungu, sio kikubwa lakini kidogo nilichokifikia
kinanisaidia sana. Wasanii sasa wanaanza kuniambia yule mwalimu wako
anaitwa nani, niunganishe na mwalimu wako nawaambia ‘it’s too late you
know.’
Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya
No comments:
Post a Comment