Thursday 8 October 2015

ROMA atangaza kuachia ngoma mpya October 25 ambayo ni siku ya uchaguzi

Baada ya kukumbana na changamoto nyingi alipoachia wimbo wake wa ‘Viva Roma Viva’, Rapper wa Tongwe Records, Roma ametangaza kuja na wimbo mpya ambao atauachia siku ya uchaguzi mkuu.

October 25 siku ambayo Watanzania watajipanga kwenye mistari kwajili ya kushiriki zoezi muhimu la kuwachagua viongozi wanaowataka, rapper Roma amepanga kuwapa wimbo mpya utakaotoka siku hiyo.

Roma ambaye amekutana na vikwazo vingi kupitia wimbo huu wa sasa VRV ikiwemo BASATA kutangaza kuufungia, ametumia mitandao ya kijamii kuwataarifu mashabiki kuhusu ujio wa wimbo mpya ambao hajasema utaitwaje.


“#ON_SET Guess what!!!!!!! MY NEW SONG loading….. Nitai#RELEASE On 25th OCTOBER” aliandika Roma. 

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya

No comments:

Post a Comment