Tuesday, 13 October 2015

Mr Blue amesema kuingia kwenye uvutaji wa bangi kulimsabisha aache shule na kutaka kukaa kijiweni

Rapper Mr Blue amesema kuingia kwenye uvutaji wa bangi kulimsabisha aache shule na kutaka kukaa kijiweni zaidi. Mr Blue aliliambia gazeti la Mwananchi kuwa, kuna vitu vingi ameshindwa kufanya kotokana na kuwa mtumwa wa bangi.

Najuta kujiingiza kwenye matumizi ya bangi,” anasema. “Siwezi kusema ni madawa ya kulevya kama inavyojulikana kwa unga na cocaine. Sijawahi kufikia huko, bali nilivuta sana bangi na pombe kali ila kwa sasa nimeacha kabisa.

Mambo mengi kwenye maisha yangu yalikuwa hayafanyiki kadri nilivyokuwa nataka, nilikuwa napoteza muda wangu kwenye kukaa kijiweni kuliko kufanya kazi,” alimalizia Blue.

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment