Friday, 16 October 2015

Hemedy PHD asema hana mpango wa kufanya video nje ya nchi


Msanii huyo wa muziki na filamu amesema kuwa hana mpango wa kwenda kushoot video za nyimbo zake nje ya nchi kama wafanyavyo baadhi ya wasanii wengine.

Staa huyo ambaye ameachia wimbo mpya ‘Memories’ hivi karibuni, amesema kikubwa ambacho anakifikiria ni kufanya kazi na wasanii wa nje lakini si kufanya video nje.

“Kitu ambacho kipo kichwani mwangu kwa sasa ni kufikiria kufanya kazi na wasanii wa nje, ili niweze kuupaisha muziki wangu kimataifa zaidi na kuweza kuitangaza vyema Tanzania, sifikirii video za nje,” alisema Hemedy

Hii ni moja ya video zake alizofanya hapa nyumbani


Source: Mtanzania

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya




No comments:

Post a Comment